Utangulizi
Ulinganifu
kati ya hadighi ya damu nyeusi, wimbo uliotiririka na ndoa ya samani.
“Damu Nyeusi” ni hadithi inayoonyesha ubaguzi wa
mtu mweupe thidi ya mtu mweusi yaani
“vita kati ya weupe na weusi. Vita hivyo vimedhihirishwa na msanii wa hadithi
hii ya damy nyeusi kwa kumtamia mhusika fikirini ambaye alibaguliwa na watu
weupe nchini marekani alipokuwa akisoma kozi yake ya ualimu yaani akiwa masomoni
alibaguliwa na wahadhiri katika upewaji wa alama na hata nje ya chuo
alibaguliwa mfano uk 23 fikirini kulipishwa faini barabarani ilihali wengine
wazungu wakiachwa pia ukurasa huohuo weusi walibaguliwa katika alama za masomo.
“Macko” ni hadithi inayoonesha
/elezea jinsi mwanamke anavyoteseka katika ndoa yake huku akipigwa na mumewe,
mwansishi amethibitisha suala hilo kwa kumtumia Jamila “mkewe hamduni” ambaye
aliteseka katika ndoa yake kwa kupata kipigo kutoka kwa mumewe (uk 51) pia
hadithi hii inaonyesha jinsi mwanamke alivyokuwa na uhaba wa elimu ya haki za
binadamu, kwani Jamila hakuwa na elimu
iliyomfanya afahamu kuwa haki zake za msingi zilikuwa zikivunjwa na mumewe kwa
kumpiga na kumnyanyasa kijinsia, hii inadhihirika pale Hamduni alipompiga mkewe
teke kwa kuchelewa kumpatia chakula. (uk 54). “Kama lile teke la mbavu
alilorushiwa Jamila eti kwa sababu hakufanya haraka kuleta chakula”
“Ndoa
ya samani” Ni hadithi inayoelezea jinsi watu/ binadamu anavyopenda mali au pesa
kuliko utu kwa mfano AMALI alipenda sana pesa kuliko utu, hii ni pale Amali na
Familia yake ilivyokataa posa ambayo
ilikutwa kwa Amali kisa mposaji hakuwa na hali nzuri kifedha yaani masikini.
Lakini baadaye ilikubaliwa posa hiyo mara tu baada ya mposaji (Abu) kuwa na
fedha alipotoka “Arabuni” uk 86.
Linganua
ama lingalisha hadithi zozote tatu kutoka Damu Nyeusi na hadithi nyingine (Ken
Walibora na Said A. Mohammed, kwa kuzingatia kipengele cha fani na maithui.
Ufuatao
ni ufanano wa hadithi ya “Damu Nyeusi” “Maeko” na Ndoa ya Samani katika
kipengele cha fani na maudhui.
Kipengele
cha fani
Fani
ni mbinu za kisanaa anazotumia mwandishi ili kufikisha ujumbe wake kwa jamii.
Fani hujumuisha wahusika, matumizi ya lugha, muundo, kulinda na mandhari.
Hadithi
hizi tatu zimefanana kifani kama ifuatayo:-
Muundo.
Hadithi zote tatu zimetumia muundo wa moja kwa moja. Ambapo visa vimesimulia
tuanzia mwanzo mpaka mwisho. Mfano, katika hadithi ya MAEKO msimuliali anaanza
kwa kusimulia kisa cha uleci wa Duni na ndoa yake mpaka mwisho, Duni
anajitambua kuwa anatenda ndivyo isivyo kwa mke wake pindi akiwa amelewa na
pindi pombe inapomwiisha huonyesha mapenzi mema kwa mkewe ambapo kisa hiki
kimeonyeshwa mwishoni mwa hadithi hii. Mfano, Uk 56 “ Nisamehe Jamila. Nisamehe
mke wangu ……….”
Muundo.
Hadithi zote tatu zimetumia muundo wa moja mpaka. Ambapo visa vimesimulia kuanzia uwezo mpaka mwisho.
Mfano, katika hadithi ya MAEKO msimuliaji anaweza kwa kusimulia kisa cha ulevi
wa Duni na ndoa yake mpaka mwisho, Duni
anajitambua kwa anatenda ndivyo isivyo kwa mke wake pindi akiwa amelewa na
pindi pombe inapomwiisha huonyesha mapenzi mema kwa mkewe ambapo kisa hiki
kimeonyeshwa mwishoni mwa hadithi hii. Mfano; 56 “Nisamehe Jamila. Nisamehe mke
wangu……..”
Hivyo
hivyo katika hadithi ya “Damu Nyeusi” msimuliaji anaweza kuwa kusimulia jinsi
Fikirini alivyoenda masomoni huko marekani na kukukutana na ubaguzi wa rangi na
mateso dhidi yake mpaka mwisho wa hadithi. Vilevile katika hadithi ya Ndoa ya
Samani” msimuliaji ameanza kwa
kumuonyesha Abu akienda kutoa mahari kwa akina Amali, anakataliwa na wazazi wa
Amali kuwa yeye wewe ni fukara, halafu anaenda uarabuni kutafuta pesa, kurudi
nyumbani na kuanza kujenga na baadae kwenda tena kwa Amali ili kumuoa
lakini mwishowe anagundua kwa Amali
amekuwa na mali yako na si yeye
aliyemuoa. Mfano (uk. 89) “Amali sidhani kapenda kuolewa name; sikuwa mimi bali ameolewa na
mali yangu”. Hivyo akiamua kumuacha na kwemda uarabuni.
Muundo.
Hadithi zote tatu zimetunia mtindo wa kufanana kwa sehemu kubwa, kwanza hadithi
zote tatu zimetumia mbinu ya masimulizi mwanzo wa hadithi mpaka mwisho wa
hadithi. Pia kuna matumizi ya nafsi ambapo nafsi zote tatu zimetumika. Mfano:
katika MAEKO anasema “maskini” Jamila machozi yalimtoka “Hii ni nafsi ya tatu mmoja (uk.51). hivyo hivyo
katika hadithi ya “Ndoa ya Samani” kuna matumizi ya nafsi ya tatu umoja katika
(uk. 87) mfano “….alikataa posa yangu”. Vilevile katika “Damy Nyeusi” (uk 25)
kwa mfano: anasema “alipokaribiana na Yule dada….”
Wahusika:
hadithi zote zimetumia wahusika ambao ni binadamu ambao majina waliyopewa na
watunzi wa hadithi zote tatu wamasadifu uhusika wao kama ifuatavyo: mfano.
Fikirini,
katika hadithi ya “Damu Nyeusi” Jina lake limemsadifu kwa ana Fikiei
tunduizi dhidi ya dhuluma za kibaguzi nchini marekani juu ya mtu mweusi
pale alipokuwa masomoni (uk.22). hivyo hivyo katika Handani au Duni katika
“Maeko” jina lake limemsadifu kuwa ni mtu
Duni. Hii ni kutokana na tabia zake za ulevi wa kupindukia ambazo ziliwafanya majirani wamdharau na kumdunisha
(uk 51) “……zikamhalalishia kabisa kuwa duni- kwa jina na maana”. Pia katika
hadithi ya “Ndoa ya Samani” Mhusika Amali amesadikiwa na jina lake
kwani Amali alikuwa ni mtoto wa pekee kwa wazazi wake na hivyo kuonekana
kuwa ni kitu cha thamani sana.
Matumizi
ya lugha. Hadithi zote zimetunia lugha yenye tamathali nyingi za semi, misemo
na pia ni lugha fasihi inayoelewela kwa wepesi.
Tamathali
za semi.
Tashiriha:
ni mbinu ya kisanaa ya kufananisha vitu viwili
tofauti.
Katika
“Damu Nyeusi” Tashibiha ifuatavyo imetumiwa na mwandishi (uk.27) “……….tumbiri
kama nyie”.
Hivyo
hivyo katika “Maeko” kuna tashibiha kama vile “ naye yakachinzika” mithili ya
maji ya mvua” (uk. 55). Pia hata katika “Ndoa ya Samani” anasema “nilikuwa nipo
kama sipo” (uk. 83).
Tafsida:
Ni mbinu ya kisanaa inayutumika ili kupunguza ukali wa maneno.
Hadithi
zote tatu zimetunia luvha ya mficho mfamo, katika “Damu Nyeusi” kuna neno
“Rabana” lemye maana ya Uchi (uk. )
ukiniba likiwa na maana ya uhusiano uk.
Pia katika Maeko tunaneno Alioteza. Lenye maana kuweka uk. Pia kuna neno
kupunapuna- kushikashika. Vilevile katika hadithi ya “Ndoa ya Samani” kuna neno
kama ulitima umaskini (uk. ) pia neno
Himu- rika (uk )
Methali
Katika
“Damu Nyeusi’ kuma methali ifuatayo “Nyumbani ni nyumbani ingawa Pangoni” (uk
2) katika “Ndoa ya Samani” kuna methali ifuatayo:-
“Atafutaye
hachoki akichoka keshapata” (Uk 86) katika “Maeko” kuna methali ifuatayo;-
“udilolijua ni usiku wa kiza” (uk 54)
Madhari/
mazingira
Hadithi
zote tatu zimetumia mandhari halisi kama ifuatayo: katika “Damu Nyeusi”
mwandishi ametumia mandhari ya nyumbani. Mfano, Pale ambapo Fikirini aliyeenda
nyumbani kwa Fiona na kufanyiwa ukatili wa namna yake (uk.29). pia katika
“Maelo” mandhari pia ya nyumbani yametumika mfano, vitendo alivyokuwa anafanya
Duni kwa Jamila yalifanyikia nyumbani kwake (uk 53). Vilevile katika “Ndoa ya
Samani’ tunaona mazingira ya nyumbani yameonekana.
Mfano:
nyumbani kwao na Amali /bibi harusi ambapo bwana harusi alivishwa mpaka
chumbani kwa bibi harusi (uk. 88) “Aligea kitandani kanipisha nikae” hapa
ilikuwa ni chumbani kwa Amali.
Kipengele
cha maudhui
Maudhui
ni jumla ya mawazo yote ya mwandishi wa kazi ya fasihi. Maudhui yanajumuisha
vipengele vifuatavyo:- Dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo na msimamo.
Dhamira
Hadithi
zote tatu zinejengwa na dhamira kuu na dhamira jenzi au mdogomdogo
Dhamira
kuu
Ujenzi
wa jamii mpya. Hadithi zote zimezungumzia ujenzi wa jamii mpya isiyo na
manyanyaso, matabaka na yenye kujali utu. Mfano: katika hadithi ya “Ndoa ya
Samani” mwandishi anaonyesha kuwa haja ya kuondoa unyanyasaji kati kati ya
walionacho dhidi ya wasionacho.
Mfano: Pale ambapo Abu kama kijana
kutoka familia maskini alizuiwa mahari kwa Amali binti kutoka familia yenye
nafasi kwa kuambiwa kwamba hataweza kutoa mahari hii inadhihirika (uk. 87)
“tena sijui kama utaweza mahari”.
Pia
katika hadithi ya “Maeko” mwandishi anazungumzia ujenzi wa jamii mpya ambayo
itamtambua mwanamke kama Jamila na kuondoa manyanyaso dhidi yake. Hivyo hivyo,
katika hadithi ya “Damu ya Samani” mwandishi ameonyesha kuwa ni muhimu kujenda
jamii isipokuwa na ubaguzi wa rangi. Hii inadhihirika katika (uk. 23) pale
fikirini anaposema “…..mtu mweusi kujikomboa kwenye mikatale ya kubaguliwa,
kubeuliwa na kudhulumiwa na mtu mweupe”
Dhamira ndogodogo
Nafasi
ya mwanamke katika jamii. Hadithi zote
tatu zimeweza kumchora mwanamke na nafsi katika jamii. Mfano, katika hadithi ya
“Damu Nyeusi” mwanamke amechorwa kama mtu katili na asiye na chembe ya huruma.
Hii imedhihirika (uk.29) pale Fiona anaposoma “Hupana usimwache aende”,
“…..kama huwezi kufyatua risasi riachiea mimi nimkale mrija” pia katika hadithi
ya “Maeko” mwanamke amechorwa kama ntu mpole, mama mwema wa familia mwenye mapendi ya dhati na mvumilivu. Mfano:
Mwandishi ameonyesha jinsi Jamila alivyo mwanamke mvumilivu katika ndoa yake
pamoja na kuwa alikuwa akipata mateso mengi kutokana na Duni kumpiga mateso na
magumu. Hii inadhihirika (uk. 53) “suala la kuachana na mumewe halikupata
kumpitikia mawazoni mwake hata siku moja na abadani asingeliwafiki shauri
hili”. Hivyo hivyo, katika “Ndoa ya Samani” mwnamke ameshorwa kama mtu
asiyekuwa na mapenzi ya kweli bali mapenzi ya pesa. Mfano: mwanzoni Amali
anakataa kuolewa na Abu kupata mali alimkubali. Hii inadhihirika katika (uk.
89) pale Abu anaposema “Amali sidhani kapenda kuolewa name, sikumuoa mimi bali
ameolewa na mali yangu”.
Kukata
tama. Hadithi zote tatu zimeonyesha hali ya kukata tama kwa baadhi ya wahusika
katika hadithi hizi. Mfano, katika “Damu Nyeusi” Fikirini alikata tama kuishi
pale alipoelekezewa na bastola yenye risasi ndani yake. Hii imedhihirishwa na
mwandishi katika (uk. 29) pale Fikirini amaposema “leo ni siku ya silu,…….siku
ya kufa, kifo cha cubu”
Pia
katika “Maeko” mwandishi aeonyesha suala hili kwa kutumia Jamila ambaye alikata
tama ya kuishi kwa starehe katika uhai wake. Hii inashihirika katika (uk. 55)
“ameshapoteza matumaini ya kuishi kwa starehe katika uhai wake” hivyo hivyo,
katika “Ndoa ya Samani” Abu alikata tama ya kumpata Amali na kuwa tena baada ya
kukataliwa posa yake aliyopeleka kwa akina Amali. (uk. 87) “Tena sijui kama
utaweza mahari”. “sikutaka kueleza jambo la ziada. Nilitamani kabisa” mjomba
wake akamwambia “usife moyo”
Migogoro.
Migogoro
ni hali ya kutokuwa na maelewano baina ya mtu na nafsi yake, mtu na mtu au mtu na
kundi Fulani.
Hadithi
zote zimeonyesha migongoro yote ambayo ni, ngogoro wa nafsi, mgogoro wa mtu na
mtu, na mtu na kundi la watu.
Katika
hadithi ya Damu kuna mgogoro baina ya Fikirini na nafsi yake. Mgogoro huu
ulisababishwa na ubaguzi wa rangi unaofanywa na watu weupe kwa waafrika. Pia
kulikuwa na mgogoro baina ya Fikirini na Fiona. Mgogoro huu ulisababishwa na
Fiona pale alipotaka begi la Fikirini ili kutaka pesa. Vilevile, kulikuwa na
mgogoro kati ya Fikirini na Jamii ya watu weupe na wamarekani weusi mgogoro
uliosababishwa na …………watu wengi waliokuwa
akifanyiwa Fikirini alipokuwa chuoni na hata nje ya chuo.
Pia
katika “Maeko” Jamila alikuwa na mgogoro wa nafsi nliotokana na mume wake kuwa mlevi wa kupindukia hali
iliyomfanya asiishi kwa furaha. (uk 51) jamila alisema hadi lini? Duni ataendelea kurudi….” Pia alikuwa na
migogoro kati yake na Salim, mgogoro huu
ulisababishwa na Salimu kumshauri Jamila
aanchane na mumewe (uk. 54). Vilevile Jamila alikuwa na mgogoro na majirani
waliomshauri aachane na mumewe (uk 53).katika hadithi ya “Ndoa ya Samani”
Mgogoro wa nafsi ulikuwa kwa Abu aliyekataliwa kumwoa Amali (uk 78). Pia Abu alikuwa na mgogoro kati yake na Amali uliosababishwa na Abu kumuoa
kutokufunga ndoa na Amali na kumuacha
chumbani Amali peke yake (uk 59). Vilevile katika hadithi hii mgogoro wa
mtu na kundi Fulani umetokea baina ya Abu na familia ya akina Amali. Mgogoro
huu unesababishwa na Abu kukataliwa kumwona Amali hali iliyompelekea alipize
kisasi kwa kumuoa kuvunja ndoa iliyotarajiwa kufungwa kati yake na Amali (uk
87).
Ujumbe
Hadithi
zote hizi tatu zinatoa ujumbe kuwa binadamu wote ni sawa, hivyo mtu asibaguliwe
wala kunyanyaswa kutokana na rangi yake, hali yake ya kifedha ama kiuchumi na
jinsia yake.
Falsafa
ni imani ya mwandishi juu ya kile anacholisimamia au anachokizungunzia.
katika hadithi zote tatu wandishi wanaamini
kuwa, ili ujenzi wa jamii mpya ufanikiwe
lazima tupige vita unyanyasaji,
natabaka na ubaguzi wa rangi katika jamii.
Mtazamo
Mtazamo
ni jinsi ambavyo mwandishi anavyoyatazama matatizo mbalimbali yanayoikabili
jamii yake kwa lengo la kutolea ufumbuzi.
Katika
hadithi hizi waandishi wanamtazamo au msimamo wa kinyakinifu ambapo wanaona
kuwa matatizo yote yanayoikumba jamii yanasababishwa na binadamu/ mwanadamu
mwenyewe kwa mfano suala la ubaguzi wa rangi ulioonekana katika “Damu Nyeusi”
umesababishwa na binadamu mwenyewe.
Msimamo
Ni
jinsi mwandishi anavyotazama mambo na kuonyesha msimamo wake juu ya kile
anachoamini kuwa ni suluhisho la matatizo katika jamii yake.
Waandishi
wa hadithi zote tatu wana msimamo wa kimapinduzi. Ambapo waandishi wanaonyesha
msimamo wao wakupinga watabaka na kuitaka jamii yao kuamka na kupiga vikwazo
vyote vya maendeleo ikiwemo matabaka na ubaguzi wa rangi ili kujenga jamii
mpya.
Marejeleo
Waambora,
K. na Mohammed S.A (2007) Damu Nyeusi na Hadithi nyingine. Moran publidhers: Nairobi, Kenya.
No comments:
Post a Comment