Thursday, July 14, 2016

DAMU NYEUSI KATIKA KITABU CHA MOHAMED S.A



Utangulizi
Ulinganifu kati ya hadighi ya damu nyeusi, wimbo uliotiririka na ndoa ya samani.
            “Damu  Nyeusi” ni hadithi inayoonyesha ubaguzi wa mtu mweupe  thidi ya mtu mweusi yaani “vita kati ya weupe na weusi. Vita hivyo vimedhihirishwa na msanii wa hadithi hii ya damy nyeusi kwa kumtamia mhusika fikirini ambaye alibaguliwa na watu weupe nchini marekani alipokuwa akisoma kozi yake ya ualimu yaani akiwa masomoni alibaguliwa na wahadhiri katika upewaji wa alama na hata nje ya chuo alibaguliwa mfano uk 23 fikirini kulipishwa faini barabarani ilihali wengine wazungu wakiachwa pia ukurasa huohuo weusi walibaguliwa katika alama za masomo.
            “Macko” ni hadithi inayoonesha /elezea jinsi mwanamke anavyoteseka katika ndoa yake huku akipigwa na mumewe, mwansishi amethibitisha suala hilo kwa kumtumia Jamila “mkewe hamduni” ambaye aliteseka katika ndoa yake kwa kupata kipigo kutoka kwa mumewe (uk 51) pia hadithi hii inaonyesha jinsi mwanamke alivyokuwa na uhaba wa elimu ya haki za binadamu, kwani Jamila  hakuwa na elimu iliyomfanya afahamu kuwa haki zake za msingi zilikuwa zikivunjwa na mumewe kwa kumpiga na kumnyanyasa kijinsia, hii inadhihirika pale Hamduni alipompiga mkewe teke kwa kuchelewa kumpatia chakula. (uk 54). “Kama lile teke la mbavu alilorushiwa Jamila eti kwa sababu hakufanya haraka kuleta chakula”
“Ndoa ya samani” Ni hadithi inayoelezea jinsi watu/ binadamu anavyopenda mali au pesa kuliko utu kwa mfano AMALI alipenda sana pesa kuliko utu, hii ni pale Amali na Familia yake  ilivyokataa posa ambayo ilikutwa kwa Amali kisa mposaji hakuwa na hali nzuri kifedha yaani masikini. Lakini baadaye ilikubaliwa posa hiyo mara tu baada ya mposaji (Abu) kuwa na fedha alipotoka “Arabuni” uk 86.
Linganua ama lingalisha hadithi zozote tatu kutoka Damu Nyeusi na hadithi nyingine (Ken Walibora na Said A. Mohammed, kwa kuzingatia kipengele cha fani na maithui.
Ufuatao ni ufanano wa hadithi ya “Damu Nyeusi” “Maeko” na Ndoa ya Samani katika kipengele cha fani na maudhui.

Kipengele cha fani
Fani ni mbinu za kisanaa anazotumia mwandishi ili kufikisha ujumbe wake kwa jamii. Fani hujumuisha wahusika, matumizi ya lugha, muundo, kulinda na mandhari.
Hadithi hizi tatu zimefanana kifani kama ifuatayo:-
Muundo. Hadithi zote tatu zimetumia muundo wa moja kwa moja. Ambapo visa vimesimulia tuanzia mwanzo mpaka mwisho. Mfano, katika hadithi ya MAEKO msimuliali anaanza kwa kusimulia kisa cha uleci wa Duni na ndoa yake mpaka mwisho, Duni anajitambua kuwa anatenda ndivyo isivyo kwa mke wake pindi akiwa amelewa na pindi pombe inapomwiisha huonyesha mapenzi mema kwa mkewe ambapo kisa hiki kimeonyeshwa mwishoni mwa hadithi hii. Mfano, Uk 56 “ Nisamehe Jamila. Nisamehe mke wangu ……….”
Muundo. Hadithi zote tatu zimetumia muundo wa moja mpaka. Ambapo  visa vimesimulia kuanzia uwezo mpaka mwisho. Mfano, katika hadithi ya MAEKO msimuliaji anaweza kwa kusimulia kisa cha ulevi wa Duni na ndoa yake mpaka  mwisho, Duni anajitambua kwa anatenda ndivyo isivyo kwa mke wake pindi akiwa amelewa na pindi pombe inapomwiisha huonyesha mapenzi mema kwa mkewe ambapo kisa hiki kimeonyeshwa mwishoni mwa hadithi hii. Mfano; 56 “Nisamehe Jamila. Nisamehe mke wangu……..”
Hivyo hivyo katika hadithi ya “Damu Nyeusi” msimuliaji anaweza kuwa kusimulia jinsi Fikirini alivyoenda masomoni huko marekani na kukukutana na ubaguzi wa rangi na mateso dhidi yake mpaka mwisho wa hadithi. Vilevile katika hadithi ya Ndoa ya Samani” msimuliaji  ameanza kwa kumuonyesha Abu akienda kutoa mahari kwa akina Amali, anakataliwa na wazazi wa Amali kuwa yeye wewe ni fukara, halafu anaenda uarabuni kutafuta pesa, kurudi nyumbani na kuanza kujenga na baadae kwenda tena kwa Amali ili kumuoa lakini  mwishowe anagundua kwa Amali amekuwa na  mali yako na si yeye aliyemuoa. Mfano (uk. 89) “Amali sidhani kapenda  kuolewa name; sikuwa mimi bali ameolewa na mali yangu”. Hivyo akiamua kumuacha na kwemda uarabuni.
Muundo. Hadithi zote tatu zimetunia mtindo wa kufanana kwa sehemu kubwa, kwanza hadithi zote tatu zimetumia mbinu ya masimulizi mwanzo wa hadithi mpaka mwisho wa hadithi. Pia kuna matumizi ya nafsi ambapo nafsi zote tatu zimetumika. Mfano: katika MAEKO anasema “maskini” Jamila machozi yalimtoka “Hii ni  nafsi ya tatu mmoja (uk.51). hivyo hivyo katika hadithi ya “Ndoa ya Samani” kuna matumizi ya nafsi ya tatu umoja katika (uk. 87) mfano “….alikataa posa yangu”. Vilevile katika “Damy Nyeusi” (uk 25) kwa mfano: anasema “alipokaribiana na Yule dada….”
Wahusika: hadithi zote zimetumia wahusika ambao ni binadamu ambao majina waliyopewa na watunzi wa hadithi zote tatu wamasadifu uhusika wao kama ifuatavyo: mfano.
Fikirini, katika hadithi ya “Damu Nyeusi” Jina lake limemsadifu kwa ana Fikiei tunduizi  dhidi ya dhuluma   za kibaguzi nchini marekani juu ya mtu mweusi pale alipokuwa masomoni (uk.22). hivyo hivyo katika Handani au Duni katika “Maeko” jina lake limemsadifu kuwa ni mtu  Duni. Hii ni kutokana na tabia zake za ulevi wa kupindukia ambazo  ziliwafanya majirani wamdharau na kumdunisha (uk 51) “……zikamhalalishia kabisa kuwa duni- kwa jina na maana”. Pia katika hadithi ya “Ndoa ya Samani” Mhusika Amali amesadikiwa  na jina lake  kwani Amali alikuwa ni mtoto wa pekee kwa wazazi wake na hivyo kuonekana kuwa ni kitu cha thamani sana.
Matumizi ya lugha. Hadithi zote zimetunia lugha yenye tamathali nyingi za semi, misemo na pia ni lugha fasihi inayoelewela kwa wepesi.
Tamathali za semi.
Tashiriha: ni mbinu ya kisanaa ya kufananisha vitu viwili  tofauti.
Katika “Damu Nyeusi” Tashibiha ifuatavyo imetumiwa na mwandishi (uk.27) “……….tumbiri kama nyie”.
Hivyo hivyo katika “Maeko” kuna tashibiha kama vile “ naye yakachinzika” mithili ya maji ya mvua” (uk. 55). Pia hata katika “Ndoa ya Samani” anasema “nilikuwa nipo kama sipo” (uk. 83).
Tafsida: Ni mbinu ya kisanaa inayutumika ili kupunguza ukali wa maneno.
Hadithi zote tatu zimetunia luvha ya mficho mfamo, katika “Damu Nyeusi” kuna neno “Rabana” lemye maana ya Uchi (uk.  ) ukiniba likiwa na maana ya uhusiano uk.  Pia katika Maeko tunaneno Alioteza. Lenye maana kuweka uk. Pia kuna neno kupunapuna- kushikashika. Vilevile katika hadithi ya “Ndoa ya Samani” kuna neno kama ulitima umaskini (uk.   ) pia neno Himu- rika (uk    )
Methali
Katika “Damu Nyeusi’ kuma methali ifuatayo “Nyumbani ni nyumbani ingawa Pangoni” (uk 2) katika “Ndoa ya Samani” kuna methali ifuatayo:-
“Atafutaye hachoki akichoka keshapata” (Uk 86) katika “Maeko” kuna methali ifuatayo;- “udilolijua ni usiku wa kiza” (uk 54)
Madhari/ mazingira
Hadithi zote tatu zimetumia mandhari halisi kama ifuatayo: katika “Damu Nyeusi” mwandishi ametumia mandhari ya nyumbani. Mfano, Pale ambapo Fikirini aliyeenda nyumbani kwa Fiona na kufanyiwa ukatili wa namna yake (uk.29). pia katika “Maelo” mandhari pia ya nyumbani yametumika mfano, vitendo alivyokuwa anafanya Duni kwa Jamila yalifanyikia nyumbani kwake (uk 53). Vilevile katika “Ndoa ya Samani’ tunaona mazingira ya nyumbani yameonekana.
Mfano: nyumbani kwao na Amali /bibi harusi ambapo bwana harusi alivishwa mpaka chumbani kwa bibi harusi (uk. 88) “Aligea kitandani kanipisha nikae” hapa ilikuwa ni chumbani kwa Amali.
Kipengele cha maudhui
Maudhui ni jumla ya mawazo yote ya mwandishi wa kazi ya fasihi. Maudhui yanajumuisha vipengele vifuatavyo:- Dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo na msimamo.
Dhamira
Hadithi zote tatu zinejengwa na dhamira kuu na dhamira jenzi au mdogomdogo
Dhamira kuu
Ujenzi wa jamii mpya. Hadithi zote zimezungumzia ujenzi wa jamii mpya isiyo na manyanyaso, matabaka na yenye kujali utu. Mfano: katika hadithi ya “Ndoa ya Samani” mwandishi anaonyesha kuwa haja ya kuondoa unyanyasaji kati kati ya walionacho dhidi ya wasionacho.
Mfano: Pale ambapo Abu kama kijana kutoka familia maskini alizuiwa mahari kwa Amali binti kutoka familia yenye nafasi kwa kuambiwa kwamba hataweza kutoa mahari hii inadhihirika (uk. 87) “tena sijui kama utaweza mahari”.
Pia katika hadithi ya “Maeko” mwandishi anazungumzia ujenzi wa jamii mpya ambayo itamtambua mwanamke kama Jamila na kuondoa manyanyaso dhidi yake. Hivyo hivyo, katika hadithi ya “Damu ya Samani” mwandishi ameonyesha kuwa ni muhimu kujenda jamii isipokuwa na ubaguzi wa rangi. Hii inadhihirika katika (uk. 23) pale fikirini anaposema “…..mtu mweusi kujikomboa kwenye mikatale ya kubaguliwa, kubeuliwa na kudhulumiwa na mtu mweupe”
Dhamira ndogodogo
Nafasi ya mwanamke  katika jamii. Hadithi zote tatu zimeweza kumchora mwanamke na nafsi katika jamii. Mfano, katika hadithi ya “Damu Nyeusi” mwanamke amechorwa kama mtu katili na asiye na chembe ya huruma. Hii imedhihirika (uk.29) pale Fiona anaposoma “Hupana usimwache aende”, “…..kama huwezi kufyatua risasi riachiea mimi nimkale mrija” pia katika hadithi ya “Maeko” mwanamke amechorwa kama ntu mpole, mama mwema wa familia  mwenye mapendi ya dhati na mvumilivu. Mfano: Mwandishi ameonyesha jinsi Jamila alivyo mwanamke mvumilivu katika ndoa yake pamoja na kuwa alikuwa akipata mateso mengi kutokana na Duni kumpiga mateso na magumu. Hii inadhihirika (uk. 53) “suala la kuachana na mumewe halikupata kumpitikia mawazoni mwake hata siku moja na abadani asingeliwafiki shauri hili”. Hivyo hivyo, katika “Ndoa ya Samani” mwnamke ameshorwa kama mtu asiyekuwa na mapenzi ya kweli bali mapenzi ya pesa. Mfano: mwanzoni Amali anakataa kuolewa na Abu kupata mali alimkubali. Hii inadhihirika katika (uk. 89) pale Abu anaposema “Amali sidhani kapenda kuolewa name, sikumuoa mimi bali ameolewa na mali yangu”.
Kukata tama. Hadithi zote tatu zimeonyesha hali ya kukata tama kwa baadhi ya wahusika katika hadithi hizi. Mfano, katika “Damu Nyeusi” Fikirini alikata tama kuishi pale alipoelekezewa na bastola yenye risasi ndani yake. Hii imedhihirishwa na mwandishi katika (uk. 29) pale Fikirini amaposema “leo ni siku ya silu,…….siku ya kufa, kifo cha  cubu”
Pia katika “Maeko” mwandishi aeonyesha suala hili kwa kutumia Jamila ambaye alikata tama ya kuishi kwa starehe katika uhai wake. Hii inashihirika katika (uk. 55) “ameshapoteza matumaini ya kuishi kwa starehe katika uhai wake” hivyo hivyo, katika “Ndoa ya Samani” Abu alikata tama ya kumpata Amali na kuwa tena baada ya kukataliwa posa yake aliyopeleka kwa akina Amali. (uk. 87) “Tena sijui kama utaweza mahari”. “sikutaka kueleza jambo la ziada. Nilitamani kabisa” mjomba wake akamwambia “usife moyo”
Migogoro.
Migogoro ni hali ya kutokuwa na maelewano baina ya mtu na nafsi yake, mtu na mtu au mtu na kundi Fulani.
Hadithi zote zimeonyesha migongoro yote ambayo ni, ngogoro wa nafsi, mgogoro wa mtu na mtu, na mtu na kundi la watu.
Katika hadithi ya Damu kuna mgogoro baina ya Fikirini na nafsi yake. Mgogoro huu ulisababishwa na ubaguzi wa rangi unaofanywa na watu weupe kwa waafrika. Pia kulikuwa na mgogoro baina ya Fikirini na Fiona. Mgogoro huu ulisababishwa na Fiona pale alipotaka begi la Fikirini ili kutaka pesa. Vilevile, kulikuwa na mgogoro kati ya Fikirini na Jamii ya watu weupe na wamarekani weusi mgogoro uliosababishwa na …………watu wengi waliokuwa  akifanyiwa Fikirini alipokuwa chuoni na hata nje ya chuo.
Pia katika “Maeko” Jamila alikuwa na mgogoro wa nafsi nliotokana  na mume wake kuwa mlevi wa kupindukia hali iliyomfanya asiishi kwa furaha. (uk 51) jamila alisema hadi lini?  Duni ataendelea kurudi….” Pia alikuwa na migogoro kati yake na Salim, mgogoro  huu ulisababishwa  na Salimu kumshauri Jamila aanchane na mumewe (uk. 54). Vilevile Jamila alikuwa na mgogoro na majirani waliomshauri aachane na mumewe (uk 53).katika hadithi ya “Ndoa ya Samani” Mgogoro wa nafsi ulikuwa kwa Abu aliyekataliwa kumwoa Amali  (uk 78). Pia Abu alikuwa na mgogoro kati  yake na Amali uliosababishwa na Abu kumuoa kutokufunga ndoa na Amali na kumuacha  chumbani Amali peke yake (uk 59). Vilevile katika hadithi hii mgogoro wa mtu na kundi Fulani umetokea baina ya Abu na familia ya akina Amali. Mgogoro huu unesababishwa na Abu kukataliwa kumwona Amali hali iliyompelekea alipize kisasi kwa kumuoa kuvunja ndoa iliyotarajiwa kufungwa kati yake na Amali (uk 87).
Ujumbe
Hadithi zote hizi tatu zinatoa ujumbe kuwa binadamu wote ni sawa, hivyo mtu asibaguliwe wala kunyanyaswa kutokana na rangi yake, hali yake ya kifedha ama kiuchumi na jinsia yake.
Falsafa ni imani ya mwandishi juu ya kile anacholisimamia au anachokizungunzia.
 katika hadithi zote tatu wandishi wanaamini kuwa, ili ujenzi wa jamii mpya ufanikiwe  lazima tupige vita unyanyasaji,  natabaka na ubaguzi wa rangi katika jamii.
Mtazamo
Mtazamo ni jinsi ambavyo mwandishi anavyoyatazama matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii yake kwa lengo la kutolea ufumbuzi.
Katika hadithi hizi waandishi wanamtazamo au msimamo wa kinyakinifu ambapo wanaona kuwa matatizo yote yanayoikumba jamii yanasababishwa na binadamu/ mwanadamu mwenyewe kwa mfano suala la ubaguzi wa rangi ulioonekana katika “Damu Nyeusi” umesababishwa na binadamu mwenyewe.
Msimamo
Ni jinsi mwandishi anavyotazama mambo na kuonyesha msimamo wake juu ya kile anachoamini kuwa ni suluhisho la matatizo katika jamii yake.
Waandishi wa hadithi zote tatu wana msimamo wa kimapinduzi. Ambapo waandishi wanaonyesha msimamo wao wakupinga watabaka na kuitaka jamii yao kuamka na kupiga vikwazo vyote vya maendeleo ikiwemo matabaka na ubaguzi wa rangi ili kujenga jamii mpya.




Marejeleo
Waambora, K. na Mohammed S.A (2007) Damu Nyeusi na Hadithi nyingine. Moran  publidhers: Nairobi, Kenya.

No comments:

Post a Comment